18 Jul 2016

Kim Kardashian amuumbua Taylor Swift kwa kuweka video Snapchat akimruhusu Kanye West amuite ‘bi*ch’ kwenye Famous



Baada ya miezi takriban miwili iliyopita Swift kudai kuwa hakumpa ruhusu Kanye West kumuita ‘bitch’ kwenye wimbo Famous, Kim Kardashian ameipost kwenye mtandao wa Snapchat video inayomuonesha mume wake huyo akiongea na Swift kumuomba ruhusu autoe wimbo huo.



Kwenye video hiyo Swift anasikika akimpa baraka zote Yeezy kuutoa wimbo huo na kumshukuru kwa heshima aliyompa ya kumjulisha kwanza.

“For all my Southside niggas that know me best / I feel like me and Taylor might still have sex / I made that bitch famous,” anarap Kanye kwenye wimbo huo.

Hata hivyo Swift amejibu kwa kudai kuwa kwenye mazungumzo hayo Kanye hakumuambia kuwa kuna mstari unaosema: I made that bitch famous.”

Kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamii, Swift amefafanua kwa kuweka maelezo yaliyotanguliwa na maneno: That moment when Kanye West secretly records your phone call, then Kim posts it on the Internet.”

0 TOA MAONI HAPA:

Post a Comment