18 Jul 2016

‘The Black Tie’ ya Wema Sepetu kumshusha Banky W wa Nigeria

Baada ya show ya ‘The Black Tie’ ya malkia wa filamu Wema Sepetu kufanikiwa weekend iliyopita, tayari mipango ya kumshusha msanii wa muziki kutoka Nigeria Banky W katika show ijayo imeanza.
Mkurugenzi wa Muna Logistics Company akiwa na Bankly W

Kampuni ya Wema Sepetu, Endless Film ikishirikiana na Muna Logistics Company imeanza kufanya mazungumzo na mkali huyo wa wimbo ‘Made For You’.

Mkurugenzi wa Muna Logistics Company, Muna kupitia ukurasa wa instagram yake amethibitisha ujio wa staa huyo.

“Unafikiri The black Tie ijayo nani anakuja kutoka nchi fulani Wema Sepetu mama mipango yako imeiva with Banky W” aliandika Muna katika picha ambayo yupo na Banky W nchini Afrika Kusini.

0 TOA MAONI HAPA:

Post a Comment